Skyner Ampa Makavu Nay wa Mitego
Msanii
wa hip hop, Nay wa mitego amechezea kichambo kutoka kwa mzazi mwenzake
ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Skyner Ally kuwa ameshindwa kuwa
baba bora kwa binti yake.
Kwenye
ukurasa wake wa instagram Skyner amefunguka maneno hayo akiwa anamtakia
heri ya kuzaliwa mtoto wake ambaye amefikisha miaka mitano na kudai
kuwa alikuwa na dukuduku kutoka moyoni ndani ya miaka mitano na baada ya
kuongea tayari limetoka.
"Thats
face you make when you see your 'daddy jina' anakufanyia promotions na
kudanganya watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi
unayovaa hajui thamani yake maskini. nimevumilia sana It's 5 Years now
nimejiskia kutapika na nimetapikaa. Am done Mungu wa mbinguni nakuomba
unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki..... uzima wa afya
nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa
nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake" aliandika Skyner.
Aidha skyner ameendelea kufunguka kuwa "Endelea
na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki...Please unapost
picha za mtoto wangu za nini...shobo dundo zanini? Sitaki shobo na
mwanangu koma kama ulivyo komaaa...Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda
watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa
nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi
Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done"- Aliongeza Skyner.
Skyner hakuishia hapo aliendelea kutoa usia kwa binti yake kwa kuonyesha jinsi alivyo na umuhimu katika maisha ya binti yake "Hakuna
anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba'ko hana
analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha
kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie
nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki
nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama
bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy
Birthday My Happiness"- Skyner alimaza
Maneno
hayo makali kwa Skyner yalikuja muda mfupi baada ya Nay kuweka picha ya
binti yake na kumtakia heri ya kuzaliwa na kudai kuwa amenunua bastola
kwa ajili ya kumlinda.

Comments
Post a Comment