Posts

Showing posts from April, 2017

BREAKING NEWS:HII HAPA ORODHA YA MAJINA YA WAFANYAKAZI WENYE VYETI FEKI MIKOA YOTE TANZANIA

Image
Habari zenu WADAU, Kama kawaida yetu FUNGUKA24 na JUNGUKUULEO ni kukupa kitu roho inapenda,tumekuwekea hapo chini orodha yenye majina ya watumishi wenye vyeti feki TANZANIA. mikoa yote na wilaya zote. WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI WENYE VYETI FEKI  << BONYEZA HAPA >> KWA WAFANYAKAZI WA TAASI ZA SERIKALI MFANO,UDSM   >> BONYEZA HAPA <<

Waziri wa Afya ataja vipimo na dawa za malaria zinazotakiwa kutolewa bure

Image
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku vituo vya Umma kuwalipisha wananchi wanaokwenda kupima maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa kipimo cha MRDT na utoaji wa dawa za mseto (ALUU) zinazotumika kutibu ugonjwa huo kuanzia sasa.

Samia Suluhu: Kero za Muungano zitatatuliwa kwa mazunguzo ya pande Mbili

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi kudumisha na kuuenzi Muungano wa Taganyika na Zanzibar na kuwahakikishia wananchi wa pande Mbili kuwa kero chache za Muungano ambazo zimebaki zitamalizwa kwa mazungumzo kama hatua ya kudumisha Muungano huo.

Mtatiro: CUF haina walinzi wa chama wenye bastola

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, The Civic United Front (CUF) Julius Mtatiro amefunguka na kusema chama cha CUF hakina walinzi wa chama wenye bastola wala hakina walinzi wanaozunguka mitaani kufanya doria.

Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi kuhusu Serikali kumuondoa nchini, Mkurugenzi wa UNDP, Bi. Awa Dabo.

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Serikali yamuondoa Mkurugenzi wa UNDP nchini    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP) kwa upande wa Tanzania kumuondoa nchini Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi Awa Dabo.

Jeshi la Polisi Lasema Linawashikilia Watu 3 Kwa Kuvamia Mkutano wa CUF na Kuwapiga Watu

Image
Saa  tatu baada ya viongozi wa CUF kukutana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, kuhoji sababu za kutokamatwa watu waliofanya vurugu kwenye mkutano wa waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho wa wilaya ya Kinondoni, Jeshi la Polisi limetangaza kushikilia watu watatu.

Polepole Aitaka CCM Imchukulie Hatua za Kinidhamu Nape Nnauye

Image
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amelaani vikali kauli iliyotolewa na mtangulizi wake ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kuwa alisaidia kukitoa chama hicho shimoni.

AWARD WINNER: N'Golo Kante reacts to being crowned the PFA Player of the Year

Image
C helsea midfielder N'Golo Kante has been voted the Professional Footballers' Association player of the year for the 2016-17 season. The Frenchman, who is on course to win a second successive Premier League title after also being part of the Leicester side which upset the odds last season, secured the most votes from his fellow players. He saw off competition from Chelsea team-mate Eden Hazard - who won the award in 2015 - plus Tottenham's Harry Kane, Everton striker Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic of Manchester United and Arsenal's Alexis Sanchez.

Tamko la serikali kuhusu kushambuliwa waandishi wa habari katika mkutano wa CUF

Image
Serikali imepokea kwa masikitiko taarifa za kushambuliwa na kujeruhiwa baadhi ya waandishi wa habari katika mvutano uliotokea juzi jijini Dar es Salaam kati ya wafuasi wa pande mbili zinazokinzana za Chama cha Wananchi (CUF). Tumechukua muda kidogo kulifuatilia suala hili na kubaini licha ya baadhi yao kujeruhiwa na kuripoti polisi, wapo waandishi ambao vifaa vyao vya kazi pia vililengwa katika shambulizi hilo.

Mgogo CUF Wazidi Kuwaka Moto......Wabunge Walaani, Polisi Wafuta Mkutano wa Maalim Seif

Image
Siku  moja baada ya kutokea kwa vurugu kubwa katika mkutano wa viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam kwa kuvamiwa na genge la watu waliokuwa na silaha za moto, wabunge wa upinzani wameibuka na kuitupia lawama Serikali.

Uteuzi wa Jokate Mwegelo UVCCM Waibua Mfarakano

Image
Uteuzi  wa Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, unaonekana kutaka kuivuruga jumuiya hiyo.

Askofu Gwajima Kununua Treni ya Umeme

Image
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amedhamiria kununu treni ya umeme baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya kujenga reli ya kisasa(standard gauge).

Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 24, 2017

Image
Tazama hapa moja kwa moja kutoka Bungeni Dodoma kipindi cha Maswali na Majibu katika Bunge la 11, Mkutano wa Saba leo Aprili 24, 2017. Bofya hapo  chini Kutazama.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 24

Image

TFF Yaipokonya Simba Pointi 3 za Kagera Sugar

Image
Hatimaye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipokonya pointi tatu Simba SC, ilizokuwa imepewa kutoka kwa Klabu ya Kagera Sugar.

Kauli ya Jerry Muro baada ya Haji Manara wa Simba kufungiwa na TFF

Image
Muda mfupi  baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya nidhamu ya TFF kutangaza kumfungia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara kwa utovu wa nidhamu na kukutwa na makosa matatu.

Skyner Ampa Makavu Nay wa Mitego

Image
Msanii wa hip hop, Nay wa mitego amechezea kichambo kutoka kwa mzazi mwenzake ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Skyner Ally kuwa ameshindwa kuwa baba bora kwa binti yake.

Msemaji wa Simba afungiwa kujihusisha na soka kwa mwaka mmoja

Image
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia Haji Manara (Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba) kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia anatakiwa kulipa faini ya Shilingi  Milioni tisa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 23

Image

Atembezwa Nusu UCHI Na Kisha Kulazimishwa Kula Kinyesi kwa Kosa la Kumtukana Mama Yake

Image
Wanawake wa kijiji cha Kisungamile kilichopo katika Kata ya Matai wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wamemwadhibu Vitus Nyami (26) kwa kumtembeza nusu uchi na kulazimisha kula kinyesi cha ng’ombe kwa kosa la kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni.

Mfanyabiashara Auawa kwa Risasi Singida

Image
Mauaji ya kutumia silaha za moto yameendelea kushamiri nchini,baada ya mfanyabiashara mmoja mjini Singida kufariki dunia baada ya kupigwa risasi ya bunduki aina ya bastola wakati akitaka kuondoka dukani kurejea nyumbani.

Mkutano wa CUF ya Maalim Seif Wavamiwa na Watu wenye Silaha......Wananchi Wafanikiwa Kumnasa

Image
Watu wasiofahamika wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.