Msemaji wa Simba afungiwa kujihusisha na soka kwa mwaka mmoja
Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia Haji Manara
(Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba)
kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia anatakiwa kulipa
faini ya Shilingi Milioni tisa.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa amesema hatua hiyo
imefikiwa baada ya Manara kukutwa na makosa matatu dhidi ya TFF ambao ni
walalamikaji.
Makosa
hayo ya Manara dhidi ya mlalamikaji TFF ni kuituhumu na kuidhalilisha
TFF, kueneza chuki za ukabila na la tatu kuingilia utendaji wa
shirikisho hilo.
Siku chache zilizopita Manara aliituhumu TFF kufanya njama za waziwazi ili kuwabeba wapinzani wao Yanga kwenye Ligi Kuu.
Manara
pia aliwatuhumu viongozi wakuu wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake,
Selestine Mwesigwa ni wahaya na viongozi wa zamani wa Yanga, ambao
wanataka kuipendelea Kagera Sugar.

Comments
Post a Comment